KLABU ya Chelsea imekuna kichwa na
kuamua kuongeza dau ili kupigania saini ya Edinson Cavani dhidi ya Paris
St Germain na sasa iko tayari kutoa Pauni Milioni 50 kwa ajili ya
kumnunua mshambuliaji huyo wa Napoli.
PSG, Laurent Blanc ametoa ofa ya Pauni Milioni 49.3 kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Uruguay.
Chelsea na Man City sasa zitatakiwa
kuvunja rekodi ya dau la usajili Uingereza, ambalo ni Pauni Milioni 50
alizotoa bilionea mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich kuilipa Liverpool
kumnunua Fernando Torres, kama wanataka kumsaini mshambuliaji huyo
gumzo kwa sasa duniani.
Cavani anatakiwa na klabu zote, lakini dau la PSG linamaanisha watatakiwa kupambana kuongeza dau kumpata mpachika mabao huyo.

Cavani alifunga dhidi ya Chelsea mwaka 2012 na wanatumai kumpata 2013

Mtu wa Pauni Milioni 50: Mshambuliaji wa
Chelsea, Fernando Torres ndiye kwa sasa anashikilia rekodi ya
kusajiliwa bei chafu Uingereza

Mifuko mizito: Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich atalazimika kutonoa mifuko yake kuipata saini ya Cavani