come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

MOURINHO AKASHIFU TUZO ZA BALLON D'OR

Jose Mourinho

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amekashifu tuzo ya Ballon d'Or inayotolewa na Fifa kwa mchezaji bora zaidi wa mwaka duniani akisema inatukuza sana mchezaji binafsi badala ya timu.

Mkufunzi huyo Mreno alijipata akiungana na meneja wa Arsenal Arsene Wenger, mkosoaji mwingine wa tuzo hiyo ambayo misimu ya majuzi imetawaliwa na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na gwiji wa Barcelona Lionel Messi.

"Ninafikiri Wenger alisema jambo ambalo ni la kufurahisha," Mourinho alisema kwenye mahojiano na tovuti ya Telegraph.
"Anapinga Ballon d'Or, na nafikiri yuko sahihi, kwa sababu kwa sasa katika soka tunapoteza dhana ya mchezo huu kuwa wa timu na badala yake kuangazia mtu binafsi.


“Huwa daima tunaangalia uchezaji wa mtu binafsi, takwimu za mtu binafsi, kwamba mchezaji fulani anakimbia zaidi. Kwa sababu unakimbia kilomita 11 katika mechi na mimi nakimbia kilomita tisa ulifanya kazi nzuri kunishinda? Labda si kweli, Labda kilomita zangu tisa ni muhimu kushinda zako 11.

“Kwangu, soka ni mchezo wa pamoja. Mtu binafsi anakaribishwa ikiwa anataka kuboresha kundi. Lakini lazima ufanyie kazi kundi, si sisi tukufanyie kazi.

“Mchezaji nyota anapofika, timu huwa tayari ipo. Si yeye anayefika na kugundua timu, kama vile Columbus aligundua Amerika. La hasha, unafika kutusaidia tuwe bora.”

Messi na Ronaldo wametawala tuzo hiyo, awali ikijulikana kama Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani, tangu 2008 na mchezaji wa mwisho ambaye hakuwa straika kushinda tuzo hiyo alikuwa difenda wa Italia Fabio Cannavaro mwaka 2006.