come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TUTAICHAKAZA MBEYA CITY KESHO- YANGA

Uongozi wa vinara wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara Yanga umesema utaendeleza vipigo kwa kila timu hadi kunyakua ubingwa wa ligi kuu msimu huu, Yanga kesho inakutana na Mbeya City ambayo katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Mbeya iliilaza mabao 3-1.


Katibu mkuu wa Yanga Jonas Tiboroha amesema ushindi kwa klabu hiyo ni kitu cha muhimu kuelekea kulirejesha taji lake la bara lililokwenda kwa Azam FC msimu uliopita, Naye msemaji wa klabu hiyo Jerry Muro amesema ni lazima ushindi upatikane hasa ukizingatia kwa sasa timu inasaka matokeo ili kuwachanganya wapinzani wao wa kombe la shirikisho Etoile du Sahel ya Tunisia.

Muro amedai baada ya timu yake kuichakaza mabao 8-0 Coastal Union itaendeleza kipigo kingine kwa Mbeya City, 'Mbeya City ya msimu huu tofauti na ile ya msimu uliopita ambayo nayo tuliifunga bao 1-0, lakini hii itegemee mabao mengi tena ikiwezekana zaidi ya Coastal Union', alisema Muro.

Kikosi cha Yanga kwa sasa hakikamatiki kutokana na safu yake ya ushambuliaji kutisha kwa mabao kwani katika mchezo uliopita mshambuliaji wake raia wa Burundi Amissi Tambwe aliweza kufunga peke yake mabao manne huku winga wake Saimon Msuva akizidi kupaa kwa upachikaji magoli