come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

ROONEY KUSAKA RAHA KWENYE DEBI

Wayne Rooney

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney ana hamu sana ya kuongezea Manchester City masaibu wakati wa debi kali itakayochezewa Old Trafford Jumapili.

Mabadiliko ya ufanisi yamepelekea United kuwa mbele ya City katika nambari tatu kwa alama moja kabla ya pambano la wikendi hii, ingawa wote wawili wako mbali sana kutoka kwa viongozi wa ligi Chelsea.

Lakini huku kukiwa na nafasi ya kumaliza nambari tatu na kufuzu moja kwa moja Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ikiwa bado inapiganiwa, debi hiyo itakuwa kali ingawa si kwamba klabu hizo mbili za Manchester zinahitaji kichocheo zaidi.


Straika wa Uingereza Rooney, 29, sasa ndiye anayeongoza United katika kufunga mabao debi hiyo akiwa na mabao 11 dhidi ya City tangu atue Old Trafford akitokea Everton 2004.

City, hata hivyo, wamekuwa wakiibuka kidedea mechi za majuzi, wakiwa wameshinda mechi nne za majuzi zaidi dhidi ya United na Rooney ana hamu sana ya kufikisha kikomo mkimbio huo.
"Unapochezea Man United, unataka sana kushinda mechi hizi za debi," aliambioa runinga na United MUTV.

“Tunataka kuwapa mashabiki wa United jambo la kuwafanya watabasamu wakirudi kazini Jumatatu asubuhi, tunataka wawe ndio watakaowacheza mashabiki wa Manchester City kazini.
“Ninafikiri ni mechi muhimu sana kwa Manchester United na Manchester City... kwa mashabiki na, kwangu, ni mechi kubwa ya fahari,” akaongeza Rooney, aliyefunga voli kali wakati wa ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Aston Villa.

Ushindi Jumapili utawaweka United alama nne mbele ya City, wanaokabiliwa na presha baada ya kushuka hadi nambari nne ligini walipochapwa 2-1 na Crystal Palace Jumatatu.

Meneja wa United Louis van Gaal anaweza kumwita raia mwenzake Robin van Persie baada ya straika huyo wa Uholanzi kurejelea mazoezi wiki hii baada ya kuumia kifundo cha mguu.
City wameshinda mechi nne pekee kati ya 11 walizocheza majuzi ligini lakini meneja Manuel Pellegrini alikiri kwamba hana wasiwasi kuhusu kazi yake.

“Huwa sina wasiwasi kuhusu kazi yangu. Huwa nafanya kazi yangu na huwa na furaha sana. Huenda ukawa na msimu mbaya, lakini huwa hutiwi wasiwasi na mambo kama haya,” Pellegrini alisema.