Liverpool inahitaji pauni millioni 20 kwa nyota wake Sterling pamoja na mchezaji wa Arsenal Theo Walcot kwa mpango huo kukubalika.
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alikuwa tayari kumuachilia Walcott kujiunga na Liverpool lakini Suarez akabadili nia na kujiunga na Barcelona.
Sasa mpango kama huo umeanza kuandaliwa huku Sterling mwenye umri wa miaka 20 akipendelea kujiunga na Arsenal naye Walcott akikosa fursa ya kuanzishwa katika kilabu ya Arsenal.