Toure ambaye yuko Equatorial Guinea akiiongoza timu ya taifa lake la Ivory Coast katika fainali za Mataifa Afrika (AFCON) zinazofanyika nchini humo badala ya Morocco iliyojitoa kwa kuhofia ugonjwa wa Ebola, amedai haelewi hatma yake ya kuendelea kuichezea Man City.
Lakini meneja wa Man City Manuel Pellegrin amesema Toure ni mali yao na ataendelea kuichezea timu yao zaidi, amedai hiki si kipindi cha kumwachia mchezaji kama huyo kwani ni muhimu katika kikosi chake, Toure amekuwa hana raha katika kikosi hicho tangia pale alipotengwa wakati wa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Toure aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa lakini hakupewa kipaumbele kama ilivyo kwa wachezaji wengine wa timu hiyo na kujikuta akilalamikia kutengwa kwake,inadaiwa vitendo vya kibaguzi ndio vimepelekea yeye kususiwa hivyo anaona ni bora aende kwingineko kutafuta amani ndani ya moyo wake