|
|
Kampeni ya kiungo maarufu mstaafu wa kimataifa wa
Ufaransa, David Ginola, kuwania urais wa shirikisho la kandanda
duniani, Fifa,dhidi ya Sepp Blatter imekumbwa na sakata baada ya taarifa
kuibuka amelipwa kusimama.
Gwiji huyo wa zamani, 47, alifichua kwamba atalipwa pauni 250,000 kuwania kiti hicho na kampuni ya Uingereza ya kucheza kamari, Paddy Power.
Ginola alitetea malipo hayo kama ‘mshahara’ wa ‘kazi njema’ akiambia runinga ya Sky Sports News, “Ni uwazi. Ni kazi, kwa nini nisiifanye? Mimi si mchezaji tena, ni kazi njema.”
“Hakuna la kutatanisha hapa, kila kitu ni wazi,” kigogo huyo alisema.
“Kimsingi, ni mshahara tu. Nalipwa kufanya kazi ya kufikia lengo la kwanza ambalo ni kuungwa mkono na mashirika matano ya kandanda na kuendeleza kampeni hadi mwisho wa Mei.”
Ikiwa Ginola atapata jina lake kwenye karatasi ya kupigia kura, anahitaji kuungwa mkono na angalau mashirika matano ya nchi wanachama wa Fifa, jambo ambalo wadadisi wengi wamepuuzilia kama ndoto tupu.
Aima yake ya kufanikiwa ilijikwaa mbele ya wanahabari aliposhindwa kutaja mwanakamati hata mmoja wa uongozi wa Fifa.