Msemaji wa Yanga Jerry Muro amesema timu yake leo itacheza kandanda la kisayansi wanalofundishwana kocha mwenye ujuzi wa hali ya juu Mholanzi Hans Van der Pluijm akisaidiana na mzalendo Charles Boniface Mkwasa.
Yanga inacheza na Ruvu Shooting ya Pwani ambayo nayo ina kumbukumbu ya kufungwa 1-0 na Mgambo Shooting wikiendi iliyopita katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, katika mchezo wa leo Ruvu Shooting ainataka kucheza kwa taadhali kubwa kwani wanaifahamu vema Yanga ambayo msimu uliopita iliwapiga mabao 7-0.
Yanga ikinolewa na Hans Van der Pluijmiliifunga bila huruma Ruvu Shooting mabao 7-0 katika mchezo wa ligi kuu bara hivyo leo hawatakubali kufungwa tena, lakini Muro amesema kipigo cha masarange hao wa JKT hakitakwepeka kwani wana hasira kubwa sana baada ya kutolewa kwenye kombe la Mapinduzi huko Zanzibar.
Muro aliyechukua nafasi ya Baraka Kizuguto amesema ushindi kwa Yanga ni jambo lililozoeleka na inapotokea imepoteza dunia nzima itasikika, sikio halivuki kichwa Yanga ni kichwa hivyo Ruyvu ni sawana masikio na wajiandae kupokea idadi kubwa ya mabao kutoka kwao.
Anasema Yanga inanolewa na kocha yule yule na falsafa yake ni kushambulia na hivi sasa timu yake ina washambuliaji hatari ambao wakikukosa basi ukatambike, lakmini msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire alisikika akisema timu yake haitakubali kufungwa na Yanga na wanaingia uwanjani kwa lengo la kulipiza kisasi, tusubiri na tuone.