come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

TAMBWE ATAJWA UFUNGAJI BORA LIGI KUU BARA MSIMU HUU

Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amewashangaa wanaosema kuwa mshambuliaji wake, Mrundi, Amissi Tambwe hawezi kuwa mfungaji bora katika Ligi Kuu Bara, msimu huu.

Tambwe ambaye amejiunga na Yanga akitokea Simba ikiwa ni siku moja kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa Desemba 15, mwaka jana, alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita kwa kufunga mabao 19 akiwa na kikosi cha Simba.

Pluijm amesema anavyomuona Tambwe ni mshambuliaji anayejiamini na mwenye nguvu ambaye analijua vizuri goli kwa hiyo msimu huu ana asilimia kubwa za kubeba tuzo ya ufungaji bora.

“Tambwe ni mshambuliaji ambaye anajiamini, ana nguvu, pia analijua goli lilipo na msimu uliopita alifanikiwa kutwaa tuzo ya upachikaji mabao, sasa kwa nini msimu huu ashindwe kufanya hivyo?” alihoji Pluijm.


Tambwe mwenyewe amekuwa akijiamini na kusisitiza hata kama si yeye kuwa mfungaji bora, bado anaamini Yanga itakuwa bingwa Ligi Kuu Bara