|
|
Kiungo nyota mzaliwa wa Ufaransa wa mabingwa wa
ligi ya Premier ya Uingereza, Manchester City, Samir Nasri atakosa ngoma
kali baina yao na klabu chake cha zamani Arsenal Jumapili kulingana na
meneja Manuel Pellegrini.
Staa huyo anatatizwa na paja kwenye jeraha litakalo mtoa mchezoni kadri majuma matatu, Pellegrini alisema Ijumaa.
“Tumekuwa na matatizo na Samir wiki hii. Nadhani atabaki nje kwa wiki tatu kwani kurudi mbele ya hapo itakuwa ngumu,” mwalimu huyo alisema.
Alizidi kuhakikishia nahodha wake na beki maarufu, Vincent Kompany na mshambuliaji matata Sergio Aguero, wako katika hali ya kuanza dhidi ya Arsenal baada ya kupata nafuu majeraha yao kikamilifu.
City wanaketi nafasi ya pili, alama mbili nyuma ya vingozi Chelsea ambao watajitosa uwanjani dhidi ya Swansea.
Wako alama 11 mbele ya Arsenal wanaomiliki nafasi ya tano.