come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

COUTINHO AMKANA MAXIMO

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Andrey Coutinho, amefunguka kuwa hajawa na mawasiliano na kocha wake wa zamani aliyekuwa anakikinoa kikosi hicho, Marcio Maximo ambaye ni Mbrazili mwenzake.

Uongozi wa Yanga ulimfungashia virago Maximo mwishoni mwa mwaka jana kwa madai kuwa alishindwa kuijenga timu vizuri huku pia akipoteza mchezo wa Nani Mtani Jembe kwa mabao 2-0 dhidi ya Simba ambapo nafasi yake imechukuliwa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

Ikumbukwe kuwa, Maximo ndiye aliyemleta nchini Coutinho pindi alipotangazwa kuwa kocha wa timu hiyo huku akimleta pia msaidizi wake Leonardo Neiva ambapo wote walitimuliwa siku moja pamoja na Wabrazili wengine, Emerson Roque na Geilson Santana ‘Jaja’.


Coutinho amesema hajawasiliana na Maximo tangu kocha huyo alipoondoka nchini Desemba, mwaka jana ambapo kwa sasa ni takribani mwezi umefika.

“Sijawasiliana naye tangu alipoondoka hapa Tanzania na hii yote inatokana na yeye kubadilisha namba yake ya simu lakini nikiipata nitamtafuta kwani yeye ni kama ndugu yangu,” alisema Coutinho.