KIKOSI cha Manchester United kimetua Bangkok na kupata mapokezi mazuri leo asubuhi, lakini wakiwa na msongo wa mawazo kutokana na habari kuhusu Thiago Alcantara.
Ilifikiriwa kwamba kiungo huyo wa
Barcelona amechagua kujiunga na United baada ya kuamua kutafuta timu
itakayomuwezesha kujenga nafasi ya kuwemo kwenye kikosi cha Hispania kwa
ajili ya Fainali za Kombe la Dunia mwakani kwa kuondoka Nou Camp.
Pamoja na hayo, sasa inaripotiwa nchini
Hispania kwamba Thiago ameona bora kwenda kuungana na kocha wake wa
zamani, Pep Guardiola huko Bayern Munich.
Sare sare: Rio Ferdinand (kushoto) na Rooney kulia
RATIBA YA ZIARA YA KUJIANDAA NA MSIMU
Julai 13 na Singha All Star XI (Uwanja wa Rajamangala, Bangkok - Kombe la miaka 80 ya Singha) saa 8mchana
Julai 20 na A-League All Stars (Uwanja wa ANZ, Sydney) sa 4.30asubuhi
Julai 23 na Yokohama F-Marinos (Uwanja wa Nissan, Yokohama) saa 5.20asubuhi
Julai 26 na Cerezo Osaka (Uwanja wa Osaka Nagai, Osaka) saa 5asubuhi
Julai 29 na Kitchee (Uwanja wa Hong Kong, Hong Kong) saa 7mchana
Ikithibitika, habari hizo zitakuwa pigo
kwa kocha David Moyes, ambaye alitumai kumtumia Thiago kuimarisha safu
yake ya kiungo, kufuatia kustaafu kwa Paul Scholes na huku Darren
Fletcher na Anderson wakiwa hawako sawa.
Mabingwa hao wa England, Manchester
United watacheza mechi tano za kirafiki katika ziara yao hii ya
Mashariki ya Mbali na Australia, wakianza na Singha All Stars Jumamosi
kujiandaa na msimu mpya, wakiwa chini ya kocha mpya, David Moyes
aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu mwishoni mwa msimu
uliopita.
kamera kamera: Kikosi cha United kilipokewa na kamera kilipotua Bangkok
Vimwana sasa: Mashabiki wa Manchester United wakiwakaribisha wachezaji wao walipotua Thailand
Mwanzo mpya: David Moyes ataanza kazi rasmi baada ya kuchukua mikoba ya ukocha United
Moyes akiwa katika hospitali Siriraj mjini Bangkok
Heshima: Moyes na Ryan Giggs wakiwa wamesimama pembeni ya picha za Mfalme wa Thai, Bhumibol Adulyadej na Malkia Sirikit
Baada ya kuondoka Uwanja wa Ndege, Moyes
na wachezaji wake walikwenda kutoa heshima zao katika hospitali ya
Siriraj mjini Bangkok. Kocha alisimama na Ryan Giggs pembeni ya picha za
Mfalme wa Thai, Bhumibol Adulyadej na Malkia Sirikit.
Kwanza Moyes akiwa na Ryan Giggs ambaye
sasa ni kocha mchezaji, walisaini kitabu cha salamu nzuri kwa Mfalme wa
Thai, ambaye anapendwa sana nchini humo.
Pia wachezaji wa United waliruhusiwa
kupumzika kwa muda baada ya saa 12 za kuwa angani kwenye ndege, na
baadaye watafanya mazoezi katika Uwanja ambao milango yote itafungwa.
Kutokana na Robin van Persie kukosa
mechi hii katika ziara hii, ambayo itaendelea Australia Jumapili kabla
ya kutua Yokohama, Osaka na kumalizia Hong Kong Julai 29, Wayne Rooney
ataanza kama mshambuliaji wa kati.
Karibu: Kikosi cha United kimepokewa vizuri Bangkok
Karibuni: Manchester United walivyopokewa Bangkok
Tabasamu la kamera: Rio Ferdinand akipiga picha za video Thailand
Wakongwe: Ferdinand (kushoto) na Ryan Giggs kulia
Pigo: Thiago Alcantara (kushoto) inadaiwa ameamua kwenda kuungana na kocha wake wa zamani, Guardiola (right) huko Bayern Munich