KILA kitu ukitaka kifanikiwe ni lazima kifanyike jijini Dar es Salaam, Huo ndio muonekano halisi tangia enzi na enzi, Ili mwanamuziki aweze kujulikana basi ahamishie shughuri zake jijini Dar taona faida yake.
Wapo wengi waliofanikiwa kimaisha kwa kupitia Dar es Salaam, Sina maana kwamba watu wote wanaotaka kufanikiwa waje Dar hapana ila njia rahisi ya kufanikiwa ipo jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa soka ni biashara kubwa sana duniani, Ukitaka kucheza soka kwa mafanikio lazima uonekane na watu wengi hatimaye jamii kukukubali, Na ili uweze kukubalika na wengi lazima uwe na watu wa kukushika mkono upande wa pili.
Lakini nyakati za nyuma tumeona wachezaji wakiondoka Dar es Salaam na kuelekea mikoani kutafuta timu ili ziweze kuwasajili kwa mashindano mbalimbali, Kipindi hicho hasa cha miaka ya tisini soka la mikoani liliweza kupiga hatua.
Nakumbuka hata mimi niliwahi kucheza soka na nilitamani sana kucheza nje ya Dar es Salaam, Kipindi hicho timu za hapa jijini zilikuwa zikisajili wachezaji toka timu za mikoani, Hivyo ni gnumu kuona mchezaji anatoka Tabora, Shinyanga au Mwanza kuja jijini Dar es Salaam kutafuta timu.
Lakini siku hizi wachezaji toka mikoani wamekuamua kukimbilia jijini Dar es Salaam kutafuta timu za kuchezea, Na hii yote inatokana na kufa kwa soka la mikoani, Miaka ya hivi karibuni soka la mikoani lilikufa kabisa.
Hakuna tena ushindnai toka kwa timu za mikoani na sijui ilitokana na nini!, Wafadhili wameacha kabisa kusaidia maendeleo ya soka mikoani tofauti na miaka ile ambapo wafadhili kadhaa walijitokeza kusaidia soka.
Ilitokea hivyo ambapo vilabu vya Simba, Yanga, Sigara hata Pilsner ziliamua kwenda mikoani kutafuta wachezaji, Hapo ndipo vijana wengi kutoka Dar es Salaam walipobahatika kurejea tena jijini kuzitumikia klabu hizo kwa jian ya kutokea mikoani.
Katika enzi zangu za kucheza soka nilikwenda mikoa ya Lindi na Pwani kusaka timu ili niweze kuonyesha makeke yangu, Nilijua Kariakoo Lindi au Reli ya Morogoro zitaniona kwa wakati ule.
Timu za Dar es Salaam kama Bom, Ashanti United, Msimbazi Rovers, Gerezani, Manyema na Vijana ya Ilala hazikuwa na thamani yoyote kwakuwa zilikuwa za Dar es Salaam, Timu zilikuwa za mikoani tu yaani Coop United ya Mwanza, Lipuli ya Iringa, Mbozi Shooting Stars ya Mbeya na nyinginezo.
Zilisifika kwa kutengeneza vipaji na matunda yake yalikuja kuonekana, Naweza kusema TFF imechangia kuua soka mikoani baada ya kutangaza kuvunja ligi za madaraja na kuunda ligi ya Taifa, Ligi ya Taifa ilionekana zaidi ya kiibepari kuliko ile iliyokuwepo zamani.
Juhudi za TFF kurejesha soka la mikoani limezidi kushindikana baada ya kushindwa kuirudisha michuano ya kombe la Taifa, Hapo sasa kumepelekea kifo cha soka la mikoani ambapo idadi ya vijana wanaoingia mjini imezidi kuongezeka kila kukicha.
Mjini kuna maendeleo makubwa kisoka kuliko vijijini, Soka limekufa kabisa kwani hakuna tena hamasa kama ile iliyokuwepo miaka ile, Simu yangu ya mkononi kila kukicha lazima nipigiwe simu angalau na mchezaji mmoja.
Simu nyingi zinazoingia zinatoka mikoani hasa kule kwenye hamasa ya mchezo wa soka ambapo kwa sasa kumesahaulika, Simba na Yanga zilikuwa zinachukua wachezaji wengi toka mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Mwanza, Morogoro na kwingineko.
Siku hizi wanachukua wachezaji 'mchangani' au kwenye hizi 'Akademia' zetu, Zote zipo jijini Dar es Salaam kama kuna nyingine nje ya jiji la Dar es Salaam basi ni ile ya jijini Arusha ya Lolingstone.
Yusuph Peter kijana aliyezaliwa 17/8/1990 mkoani Mwanza ambapo mwaka 2000 alilazimika kuhamia mjini Shinyanga na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Twende Pamoja, Sekondari alisomea Mwamalili zote zikiwa Shinyanga.
Peter ana kipaji cha kusakata kandanda na alianza kucheza soka akiwa na miaka mitano, Akizungumza na Mambo Uwanjani, Peter amesema kuwa alianza kucheza soka akiwa mdogo na sasa anataka kujiendeleza zaidi.
Mwaka 2009 Peter alishiriki katika michuano ya Copacocacola ambayo ilifanyika ngazi ya mkoa, 'Nimecheza Copacocacola mwaka 2009/10 na mimi nikicheza nafasi ya ushambuliaji yaani straika, Baadaye nikachezea timu ya shule katika michuano ya Meya ambapo niliendelea kuonyesha kipaji changu', alisema na kuongeza.
Aidha Peter ameweza kumudu nafasi nyingi uwanjani yaani kiraka, Amecheza namba kumi hadi akabilishwa namba na kuwa beki wa upande wa kulia, Katika michuano ya Meya timu yake ya shue iilikamata nafasi ya pili.
Pia alichezea timu ya kata na kufanya vizuri, Kwa sasa Peter anaomba asaidiwe, 'Naomba nisaidiwe nina kipaji kikubwa cha kucheza soka, Sitaki maneno mengi nipeni timu tu muone kipaji changu', alisema.
Aliongeza mazingira ya soka la vijijini halimpi nafasi ya kuonyesha kipaji chake, Ili kuendeleza kipaji chake anahitaji kucheza soka kwenye timu za miji iliyoendelea kama Dar es Salaam, Hivyo amezitaka klabu mbalimbali kumchukua ili anusuru kipaji chake ambacho kipo hatarini kufa.
Aidha kijana huyo analitaka shirikisho la kandanda nchini kujaribu kutembelea vijijini ambapo anadai kuna wachezaji wazuri na wanafaa kuzichezea timu za taifa, Mfano kama yeye ana kiu kubwa ya kuisaidia nchi yake ambayo bado inasuasua katika nyanja za kimataifa
Makala hii imeandikwa na Fikiri Salum