Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, ilisema kuwa kiingilio hicho ni kwa viti vya kijani ambavyo idadi yake ni 19,648 katika uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000.
"Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 kiingilio ni Sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni Sh. 10,000," ilisema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza: "Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni Sh. 15,000 wakati Sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160 na VIP A inayobeba watazamaji 748 kiingilio chake ni Sh. 30,000."
"Tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo," ilisema taarifa hiyo na kuongeza kuwa tiketi itaanza kuuzwa Ijumaa.
Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya mwisho ya kuwania tiketi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini itachezeshwa na mwamuzi Thierry Nkurunziza kutoka Burundi. Mechi ya marudiano itachezwa jijini Kampala kati ya Julai 26 na 28 mwaka huu.