NYOTA wa uzito wa juu wa Arsenal wamerejea mazoezini jana asubuhi huku kikosi cha Arsene Wenger kikianza maandalizi ya msimu mpya.
Na The Gunners wakielekea kwenye kampeni
ya kushinda taji la kwanza kwa zaidi ya miaka nane, wachezaji walifanya
mazoezi mepesi ya kukimbia na kunyanyua vitu vizito katika Uwanja wao
wa mazoezi wa Colney, London.
Mashabiki wa Arsenal watamuona Jack
Wilshere akifanya mazoezi kikosini, na wengi wakiamini uimara wa nyota
huyo wa England ni dalili nzuri kwa kikosi cha Wenger kuelekea msimu
mpya.
Kunyanyua uzito: Theo Walcott 'akipiga chuma'
Furaha ndani ya gym: Jack Wilshere na Emmanuel Frimpong wakiwa kwenye mazoezi ya kunyanyua vitu vizito
Maelekezo: Arsene Wenger akiwapa maelekezo vijana wake jana asubuhi
Kulainishwa viungo: Kocha wa mazoezi ya viungo wa Arsenal, Tony Colbert akimshughulikia Alex Oxlade-Chamberlain
Anatazama: Maroune Chamakh akiangalia mazoezi Uwanja wa Colney
Mambo poa: Lukasz Fabianski na Ryo Miyaichi wakikimbia huku Oxlade-Chamberlain akinyanyua vitu vizito