Oneal alianza kwa kuwatembelea wazazi wa Feza
nyumbani kwao na kulipa posa kwa ajili ya ndoa. Kabla ya zoezi hilo
Oneal alianza kwa kumuomba Feza kwa pete ya uchumba. Binti huyo
alipokubali ndipo ndoa ya kimila ikafanyika.
Akiwa ameambatana na mjomba wake Elikem na Angelo,
alikuwa amevalia mavazi ya Kimasai akiwa kama mfalme wa Afrika. Dada wa
Oneal alikuwa Fatima na mama yake alikuwa Natasha huku shangazi akiwa
ni Annabel aliyemaliza taratibu zote za kindoa.
Mambo yote yalikwenda kama yalivyopangwa kabla
baba wa bwana harusi, Sulu alipolipia mahari na wakafanya makubaliano
ikiwa ni pombe na vinywaji vingine vilitumika katika kumaliza zoezi
hilo.
Mama wa bwana harusi, Natasha alikuwa makini
katika kumwelekeza mwanaye namna gani ya kumuongoza binti huyo katika
maisha yao, huku dada wa Oneal Fatima akiendelea na kazi zingine. Pia
katika jumba la Diamond Hakeem alifanya tendo hilo kwa Cleo na kumuomba
kumuoa na Cleo alipokubali ndoa ikafanyika.
Wiki hii Angelo, Bimp, Cleo, Fatima, Hakeem,
Nando, Pokello wapo katika kaango la kupigiwa kutolewa wiki hii.
Kumpigia kura Nando unaandika neno VOTE kisha NANDO kwenda namba 15456
kupitia mitandao ya Zantel, Airtel, Vodacom na Tigo. Unaweza kumpigia
kura kila baada ya saa nane na kila sms itakugharimu kiasi cha Sh600 tu.