KLABU ya Barcelona imetangaza ofa ya Pauni Milioni 30 kwa ajili ya beki David Luiz – lakini Chelsea itagoma kumuuza kwa bei hiyo.
Barca, ambao pamoja na ubora wao wote,
wana hasara katika safu ya ulinzi, wanatarajiwa kuboresha ofa hiyo kwa
ajili ya beki huyo mwenye kipaji ambao wanataka awe mbadala wa Nahodha
wao, Carles Puyol.
Vyanzo vimesema ni 50/50 kwaLuiz kubaki
Chelsea, ambako amekuwa mchezaji tegemeo tangu awasili Januari mwaka
2011 akitokea Benfica, au kuhamia kwa timu hiyo kubwa Ulaya.
Wanamsubiri: Luiz anaweza kucheza pamoja na Gerard Pique na Neymar Camp Nou
Pamoja na uwezekano wa kuungana na
Gerard Pique au Puyol katika safu ya ujlinzi, Luiz pia atakwenda kufanya
kazi na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Brazil akina Dani Alves
na Neymar katika mfumo ambao anauwezea na unampendezea.
Msimu uliopita Barca iliteseka kutokana
na Puyol kuwa nje kwa sababu ya maumivu, hivyo ikawalazimisha viungo
Javier Mascherano au Alex Song kuhamia kwenye uinzi, hivyo Luiz kwa
uwezo mkubwa hivi sasa ni mtu sahihi kwao.