come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

SUALEZ AITOSA LIVERPOOL, AITAKA ARSENAL KUCHEZA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Anaenda Arsenal? Suarez anataka
kucheza Ligi ya Mabingwa
HATIMAYE Luis Suarez ametaja sababu halisi ya kumfanya atake kuondoka Liverpool.

 ni kutaka kucheza Ligi ya Mabingwa. Mshambuliaji huyo awali alisema katika mahojiano na Televisheni ya Uruguay kwamba alitaka kuondoka kuandamwa na vyombo vya Habari England na adhabu kali za FA kwa kumtuhumu kumfanyia hila za ubaguzi beki wa Manchester United, Patrice Evra na kumng’ata Branislav Ivanovic wa Chelsea. 


Lakini wakala wake, Pere Guardiola amekutana na kocha wa Wekundu hao, Brendan Rodgers na Mkurugenzi Mkuu, Ian Ayre kwenye viwanja vya mazoezi vya Melwood jana na kusema kukosa nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya imekuwa sababu kubwa kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutaka kuondoka. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema yuko tayari kutoa Pauni Milioni 30 kwa ajili ya Suarez, lakini Kop wamemuambia zitahitajika Pauni Milioni 40 ili kukaa mezani kuzungumzia dili hilo. Real Madrid pia inamtaka Suarez.