Waziri Mkuu David Cameron na Malkia Elizaeberth ni miongoni mwa
watu mashuhuri walitoa pongezi zao kwa Andy Murray baada ya kutwaa
ubingwa wa Wimbledon.
Murray mwenye miaka 26, amekuwa Muingereza wa
kwanza kwa wanaume kutwaa ubingwa huo tangu Fred Perry aliposhinda mwaka
1936, ikiwa ni zaidi ya miaka 77, baada ya kumchapa Novak Djokovic kwa
6-4, 7-5, 6-4.
Waziri mkuu Cameron aliimbia BBC: “Ulikuwa ni
mchezo wa kiwango wa Andy Murray, lakini ilikuwa ni siku nmzuri kwa
tenisi Uingereza na Waingereza pia. Hakuonyesha kukata tamaa ni jambo
zuri. “Ni fuaraha kuangalia mechi ambayo Andy Murray amekiweka historia
mpya.”
Mtangazaji wa BBC kutoka familia ya kifalme, Peter
Hunt alisema: “Malkia amemtumia ujumbe binafsi Andy Murray.” Mwendesha
baiskeli Sir Chris Hoy, mshindi wa Olimpiki kama Murray, alikuwepo
Centre Court kushudia tukio hilo la kihistoria.
“Ni fahari kushudia ushindi huu ukiwa uwanjani
pamoja na familia yako na marafiki zao, ulikuwa ni wakati maalumu,”
alisema. Amekuwa Mskochi cotland wa kwanza kutwaa ubingwa wa
Wimbledon kwa mchezaji mmoja mmoja tangu Harold
Mahony alipofanya hivyo mwaka 1896, na Mwingereza wa kwanza tangu Perry
alipochukua ubingwa huo kwa mara ya tatu mwaka 1936. Binti ya Perry,
Penny Perry, alisema anajivunia mafanikio makubwa aliyopata Murray
katika fainali hiyo.
Alisema: “Sina uhakika nilikuwa nawaza nini.
Nilikuwa nitazama huku nikiwa siamini kilichotokea. Niliduaa. “Baba
mwenyewe angefurahi.
Sisi kama familia na taifa zima tulisubirli kwa
muda mrefu, hatimaye tumefanikiwa kupata kile tulichokuwa tukisubirli
kwa muda mrefu.”
Mshambuliaji wa zamani wa England, Gary Lineker na
kocha wa zamani wa Liverpool, Kenny Dalglish ni miongoni mwa watu
waliomtumia pongezi Murray.
Gary Lineker alisema katika Twitter: “Jitihada, kipaji, kujiamini, kumeleta ushindi! Hongera bingwa wa Wimbledon!”
Dalglish aliongeza: “HuUwezi kuamini. Ni habari njema. Ni kipigo sahihi kwa mpinzani wake. Sasa ni wakati wa kushangilia.”
Beki wa Manchester United, Rio Ferdinand alisema: “Ukijituma utafanikiwa tu. Hongera Andy Murray umestahili ufalme.”