“Mashali hanipi mawazo hata kidogo, tena kwa
kumshauri kwa ngumi anazocheza bora akaombe kazi ya kupika chapati au
mandazi hotelini,” alisema Maugo jana kwenye mahojiano na Mtandao huu
Maugo na Mashali watapanda ulingoni Agosti 30
kuzichapa kuwania ubingwa wa WBF Afrika kwenye uzani wa Ssuper middle kg
76 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambapo pia
Francis Cheka atacheza na Derick Findley wa Marekani huku Alphonce
Mchumiatumbo atazipacha na De Andre McCole wa Marekani katika uzani wa
juu pambano la raundi 10.
“Sina presha ya mazoezi hivi sasa kwa ajili ya
Mashali, ni bondia mdogo mno kwangu yule namfanyia mazoezi ya siku tano
tu yanamtosha, hanipi homa hata kidogo, muacheni aropoke anavyotaka mimi
sasa hivi sitaki kuongea sana nitaonyesha vitendo ulingoni,” alitamba
Maugo.
Bondia huyo aliyevunja rekodi ya kuwa na maneno
mengi kwa mabondia wa Tanzania aliendelea kubainisha kuwa mpinzani wake
huyo siku hiyo atamtambua vizuri yeye ni bondia wa aina gani.
“Alipocheza na Cheka akawa anadondoka dondoka
hajakoma sasa namvunja mbavu, anajifanya anafanya mazoezi viwanja vya
chuo kwa ngumi gani anazocheza sana akaombe kazi ya kupika chapati
hotelini,” aliponda bondia huyo.
Akizungumzia pambano lake la Russia dhidi ya
Movsur Yusupovka litakalofanyika Julai 27 kwenye ukumbi wa Trade
&Intertainment uliopo mjini Kaspiysk, Maugo alisema yuko fiti na
kusisitiza anategemea matokeo mazuri.
“Naondoka Jumanne ijayo nchini ambapo nitakwenda
moja kwa moja Russia tayari kwa pambano hilo,” alisema Maugo na kuongeza
kuwa atakaporejea atapumzika kwa muda kabla ya kufanya mazoezi ya siku
tano.