MATUMAINI ya kocha Arsene Wenger kukamilisha uhamisho mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez yanazidi kukua.
Licha ya mwanasoka huyo wa kimataifa wa
Uruguay kusema anataka kuondoka Ligi Kuu, The Gunners wameambiwa Suarez
yuko tayari kujiunga nao majira haya joto.
Wenger amepewa ruhusa na bodi yake kutoa dau la Pauni Milioni 40, ambayo inaweza kuwa jaribio la kuuvunja Mkataba wake.

Mkwanja mnene: Arsene Wenger amepewa ruhusa kutumia Pauni Milioni 40 kwa ajili ya Luis Suarez
Liverpool inatakiwa kusikiliza ofa
itakayotolewa ya kiwango hicho na zaidi — pamoja na klabu ya Anfield
kusema kwamba hiyo haimaanishi wanalazimishwa kumuuza — na Arsenal
watatakiwa kwenda kuwaona wakiwa na Pauni Milioni 50.
Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers
anaendele kutilia mkazo Suarez hauzwi na ataweka wazi mipango yake
atakapokutana uso kwa uso na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 2 kwa
mazungumzo majira haya ya joto.
Mshambuliaji huyo ambaye hafurahiii maisha anajiandaa kwenda Montevideo kuungana na kikosi cha Liverpool mjini Melbourne kesho.
Licha ya maneno mengi ya Arsenal juu ya
dhamira yao ya kumsajili Suarez, Liverpool imepokea ofa moja tu ya Pauni
Milioni 35, ambayo imepigwa chini.

Pendeza: Mashabiki wa Liverpol wakiangalia mazoezi mjini Jakarta
Liverpool, ambayo itamenyana na Indonesian XI mjini Jakarta, itakaa kwa siku nchini Australia wiki ijayo, kabla ya kwenda Bangkok ambako wanatumai kumshawishi Suarez kuondoa mawazo ya kuondoka.
