ZAITUNI OMARI MRAPI
KWA mahesabu ya haraka haraka Yanga ndio klabu kubwa kuliko vilabu vyote Tanzania, Imezaliwa mwaka 1935 na pia ndiyo timu yenye mashabiki wengi katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati.
Inakadiriwa watu milioni kumi wanaipenda Yanga, Lakini shabiki mmoja tu yupo Ifakara mkoani Morogoro anaongoza kwa vituko kuliko wote wanaoipenda timu hiyo inayovalia jezi zake za rangi ya kijani, njano na nyeusi.
Zaituni Omari Mrapi (Pichani) alianza kuipenda Yanga tangia akiwa mgongoni mwa mama yake mzazi, Aliwashangaza wengi kwa kupenda vitu vyenye rangi ya njano na kijani na kama ukimpa rangi nyekundu huanza kulia.
Shabiki huyo alimfanya mama yake kununua ndoo za maji zenye rangi ya njano na kuzitupa zile zenye rangi nyekundu, Na ikitokea siku moja ameumia na kutokwa na damu basi hulia mpaka kuzirai kutokana na kutoipenda kabisa rangi nyekundu.
Kwa bahati mbaya baba yake mzazi alikuwa shabiki mkubwa wa Simba lakini aliamua kununua mavazi ya njano na kijani kutokana na mtoto wake kutoipenda nguo nyekundu, Baba yake huyo alilazimika kukaa naye mbali kwani mwanaye hakupenda habari zozote zinazohusu Simba.
Hakujua kama Simba ni timu isipokuwa alipata kufahamu kuwa Simba ni mnyama mkali na anaishi porini, Alipopata umri wa kuanza shule Zaituni alianza kujenga mapenzi na mchezo wa soka na timu yenye kuvaa jezi za njano ndio ilikuwa timu yake.
Hivyo alianza kupewa utamaduni na majirani pamoja na marafiki zake hatimaye kuanza kuipenda Yanga, Shabiki huyo aliendelea na mapenzi yake kwa Yanga na ilifikia hatua kudai kuwa mwanaume atakayemuoa lazima awe Mwanayanga.
Mbali ya kuipenda Yanga, Zaituni pia amelkuwa na mapenzi na Chama Cha Mapinduzi CCM, Kwa sababu wanatumia rangi inayofanana na klabu yake ya Yanga, Mnazi huyo wa kutupwa alipoamaliza masomo yake alijikita kwenye ushabiki wa soka na sasa alianza kwenda kuitazama Yanga viwanjani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Zaituni alisema kuwa mechi yake ya kwanza ilikuwa kati ya Yanga na Mtibwa Sugar iliyochezwa kwenye uwanja wa Manungu Turiani, Katika mche\o huo ambapo Yanga ilihitaji ushidni ili iweze kutetea ubingwa wake wa bara ilijikuta ikilala mabao 4-2 na kuambulia nafasi ya pili huku Mtibwa ikitawazwa mabingwa wapya wa bara.
Shabiki huyo alimwaga kilio uwanjani, Anasema kuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kuitazama Yanga na kupokea kipigo kikubwa, Siku hiyo hakuwa na furaha na alionekana mnyonge wiki nzima.
Mechi yake nyingine aliyofanikiwa kuitazama ni ile kati ya Yanga na Simba ambapo Simba ilishinda 1-0 kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro goli likifungwa na Uimboka Mwakingwe, Kusema kweli alizimia na kuwahishwa hospitali kwa matibabu.
Aliwekewa dripu ya maji na kuruhusiwa, Baadaye Yanga ilichomoza na ushindi na siku inayoshinda Yanga Zaituni huwa na furaha sana, Kwa sasa ameolewa sikia mkasa ndani ya familia yake.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Zaituni alikorofishana na mumewe baada ya kumtaka aache ushabiki wa soka, Mmewe aliona kama ndoa yake iko shakani aliamua kumpiga stop, Hapo kulipelekea kuondoka Ifakara na kutimkia jijini Dar es Salaam.
Lakini anadai anampenda sana mumewe na hakufurahishwa hata kidogo na uamuzi aliouchukua, Lakini yeye anaipenda zaidi Yanga na hakuona kama anatendewa haki kuiacha timu hiyo.
Bahati nzuri wasmaria wema waliweza kukaa meza moja yeye na mumewe na kuweza kuwapatanisha na hatimaye sasa wapo tena pamoja, Wamebahatika kupata watoto wawili ambao ni Paza (15) na Maria (4).
Zaituni anasema watoto wake wote ni mashabiki wa Yanga na siku Yanga ikishinda wanafanya sherehe kubwa, Zaituni anauomba uongozi wa Yanga umtembelee nyumbani kwake Ifakara kwani yeye ni sehemu muhimu ya Yanga.
Ana mengi ya kuwaambia viongozi wa Yanga na hasa hataki kuona timu hiyo ikifungwa na mtani wake wa jadi Simba, Hataki kuzungumzia kipigo cha goli 5-0 na Simba kwani huenda kikarudisha upya hasira zake.
Anaridhishwa na kikosi cha sasa cha Yanga na anashauri sana arejeshwe haraka Hamis Kiiza kwa anamnyima usingizi, Anafurahishwa na Abdallah Bin Kleb kwa maamuzi yake ya kuibomoa Simba na anamtaka aongeze juhudi na wala asikate tamaa.
Anakiri kiwango cha Tanzania bado kipo chii katika soka la kimataifa lakini kama vijana watawezeshwa inawezekana siku za usoni Tanzania ikawa miongoni mwa mataifa bora katika ulimwengu wa soka.
Anapenda zaidi soka kuliko michezo mingine na kinachomchosha ni kutokuwepo kwa msisimko, Anasema soka lina mashabiki wengi sehemu mbalimbali duniani na ndio maana analipenda.
Rais Kikwete amekuwa akimfurahisha sana baada ya kujitolea kwake kusaidia michezo, Anasema kuwa ukaribu wa Kikwete unamvutia sana na hakuona makosa yeye kupenda soka, Licha ya kukutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wanawake wenzie hasa wakitaka aachane na soka.
Marafiki zake wakubwa ni wanaume lakini ushabiki tu na wala si mzuka wa mapenzi, Mapenzi yake yapo kwa mumewe, Kwa sasa Zaituni amepewa dhamana kubwa na wapenzi na mashabiki wa Yanga Ifakara baada ya kumpa uongozi,
Anasema kuwa yeye ndiye mwenyekiti mwenza wa tawi la Yanga la Asante Afrika lenye wanachama 55
