![]() |
|
|
|
Kocha wa Manchester United David Moyes alisema Ijumaa
kwamba anatumaini kuwa Robin van Persie ataifaa sana klabu hiyo katika
msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza sawa na alivyofanya alipoichezea
mara ya kwanza msimu uliopita.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa kutoka Uholanzi alifanikiwa sana Old Trafford msimu uliopita baada ya kuhamia huko kutoka Arsenal na aliibuka mfungaji mabao bora zaidi wa ligi hiyo kuu Uingereza, akiwa na magoli 30 kutoka kwa mechi 48.
Moyes, ambaye amechukua usukani Manchester United baada ya kustaafu kwa meneja aliyeshinda mataji 13 ya EPL Alex Ferguson, alisema anasisimuliwa sana na kuwepo kwa van Persie katika timu yake ya kwanza msimu mpya utakapoanza kwa mechi dhidi ya Swansea City Agosti 17.
Van Persie alijunga na ziara ya timu hiyo ya kabla ya msimu wiki hii tu mjini Sydney baada ya kutokuwepo wikendi iliyopita timu hiyo ilipocharazwa 1-0 na Singha All-Star XI ya Thailand mjini Bangkok na anatarajiwa kutoa benchi na kucheza mechi ya Jumamosi dhidi ya All Stars ya Ligi-A nchini Australia.
“Tumefurahia kuwa naye hapa. Alijiunga nasi tulipofika Sydney, amefanya mazoezi kiasi binafsi,” Moyes aliambia kikao na wanahabari.
"Nasubiri kwa hamu na ghamu kumuona akianza kwenye mechi na kuwa akicheza. Alikuwa mchezaji muhimu sana kwa Manchester msimu uliopita na tunatumaini kuwa atafaa sana tena msimu huu.
“Nilipata fursa ya kukutana naye wiki hii kwa mara ya kwanza na nakwambia uwezo wake wa kudhibiti, ufahamu wake, kwenye mechi ndogo tu tulizocheza wiki hii, wacha tu,” akaongeza.
“Nimefurahishwa sana na uchezaji wake wa kitaalamu, vile anavyofanya mambo yake, amefanya mazoezi sana wiki hii.”
Moyes alisema anataka kuwezesha van Persie kufikia kilele cha uwezo wake wa kucheza.
"Kwa hivyo, yale ambayo tunafanya sasa ni kumuweka katika hali ambayo yuko tayari kufanya mambo tena kama alivyofanya msimu uliopita ambayo yalikuwa ni kufungia Manchester United magoli na alifaa sana timu. Kwa hivyo, tunatarajia kupata manufaa zaidi kutoka kwake msimu huu,” akasema.
Moyes alisema anapanga kumtumia van Persie katika kipindi cha pili cha mechi za United ziara ya kabla ya msimu nchini Australia, Japan na Hong Kong kumfanya awe katika hali nzuri tayari kwa ligi mpya.
Kiungo wa kati wa United Michael Carrick alisema van Persie ni mchezaji aliyesaidia sana timu hiyo.
"Alijiunga nasi na akaanza kucheza kwa kishindo na akatusaidia kushinda mechi muhimu na akaendelea kutoka hapo,” Carrick alisema.
"Kwetu wachezaji kuona hilo, bila shaka kukiwa na magoli mengi, lilikuwa jambo la kutia moyo sana na kwenye ligi alisaidia sana akafaa sana msimu wake wa kwanza katika klabu hii.”
Carrick aliongeza kuwa United chini ya Moyes watakuwa bora zaidi kukabili vitisho kutoka kwa Manchester City na Chelsea miongoni mwa timu tano au sita nyingine zinazopigania taji.
"Ukizingatia kwamba sisi na City na Chelsea tumebadilisha makocha kuna hisia tofauti lakini wote wana vikosi thabiti. Timu bora humaliza juu ligini na tuna matumaini tutakuwa huko,” akasema.
"Lakini kitakuwa kibarua kigumu kwani kuna timu kama tano au sita hivi ambazo zinalenga taji, au labda nambari ya pili au tatu, kwa hivyo tutahitajika kuwa bora zaidi.”