DIDIER DROGBA MATATANI, ADAIWA KUDHULUMU MAMILIONI
MAHAKAMA
Ufaransa imemuagiza mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier
Drogba kulipa Euro 450,000 kwa kampuni ya ujenzi ya mjini Corsica baada
ya kutoilipa kwa kumfanyia kazi mjini mjini Abidjan.
Kampuni
ya Acqua Viva ilimfikisha kortini mshambuliaji huyo wa zamani wa
Chelsea Mei kwa kugoma kulipa salio la malipo baada ya kujengewa nyumba
ya kifahari iliyokamilika mwaka 2009.
Kampuni
hiyo imelalamika pia wafanyakazi wake kuzuiwa kufika eneo la nyumba
hiyo waliyojenga, kitu ambacho Jaji amesema si haki na kwamba kilitokana
na maelekezo ya Drogba na mkewe, raia wa Mali, Lala Diakite.
Wakati
mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 35,
aliyejiunga na Galatasaray ya Uturuki mapema mwaka huu, ameamua kukata
rufaa, lazima alipe fedha hizo mapema ili kutekeleza amri ya Mahakama.