come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DOGO ASLAY KUJA NA 'BADO MDOGO'

BAADA ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Naenda Kusema kwa Mama’, kinda wa muziki wa kizazi kipya nchini, Asilahi Isihaka ‘Dogo Aslay’(Pichani), amefunguka juu ya uhalisia wa wimbo wake mpya wa ‘Bado Mdogo’, aliomshirikisha mwanadada Estelina Sanga ‘Lina’.


Wimbo huo ambao unazungumzia mama anayependa kufuatilia watoto wadogo na kuwataka kimapenzi, tayari umeanza kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio kutokana na ubora wa mashairi yake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dogo Aslay alisema wimbo huo ni kwa ajili ya kuwaelimisha vijana juu ya masuala hayo, lakini pia ni stori ya kweli iliyomtokea yeye akiwa na miaka 16 pale tu alipotoka na ngoma yake ya kwanza ‘Naenda Kusema kwa Mama’.

“Mimi nataka tu kuwaambia vijana wenzangu kwamba, usiombe yakukute mambo haya, wewe yasikie tu kwa watu, huo wimbo ni historia ya kweli na ukimuangalia mama mwenyewe hata mama yangu mzazi hamkuti kiumri,” alisema.

Aidha, aliwataka wapenzi wa kazi zake kumpa sapoti katika kazi zake zilizopita, pamoja na zinazokuja na kwamba, wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuipokea video ya ngoma hiyo ambayo inafanya vizuri katika chati ya muziki huo.