KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall, amesema sababu iliyofanya kumtema
mchezaji wake, Abdi Kassim ‘Babi’, ni kutokana na umri kuwa mkubwa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Hall alisema umri ndio umemuondoa Babi Azam, kwa kuwa akili ilikuwa inataka ila mwili hautaki.
“Babi alikuwa mchezaji mzuri sana, ila umri umekwenda ndiyo sababu kubwa ya kuachana naye,” alisema Hall, kocha aliyeipa Azam FC mafanikio lukuki, ikiwamo kushika nafasi ya pili Ligi Kuu Bara.
Aidha, Hall alisema kikosi chake kwa sasa kimejaa vijana wenye umri wa wastani, ambao wataisaidia timu hiyo kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine, Hall alibainisha kuwa sababu ya kutofanya usajili kwa msimu ujao ni kutokana na kuwarejesha kundini nyota wake, Aggrey Morris, Erasto Nyoni na Said Mourad, ambao anawaona kama wapya katika kikosi chake kutokana na kukaa nje muda mrefu.
Aliongeza kuwa ana imani msimu ujao timu yake itatwaa ubingwa wa Bara na kufanya vema katika michuano ya kimataifa tofauti na mwaka huu, kwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo.