![]() |
|
|
|
Sofapaka walitwaa ushindi wa 3-2 dhidi ya wageni Bandari
katika mechi ya kusisimua ya Ligi Kuu Kenya iliyosakatwa katika uga wa
Nyayo, Nairobi, Jumamosi na kupanda hadi nafasi ya tatu.
Ulikua ni ushindi wa kwanza wa Sofapaka katika mechi tano na vijana hao walilipisha kisasi cha kunyolewa 2-1 na wanabaharia hao katika mkondo wa kwanza Mombasa.
Mkwaju wa hima kutoka Felly Mulumba nusura upatie Sofapaka uongozi dakika mbili tu ndani ya mchezo pale ulipoponyoka kutoka chuma la lango.
Dakika nne baadaye, Hillary Echesa aliwatunuku uongozi baada ya ngome ya Bandari kuduwazwa na mchezo safi kati ya Bernard Mangoli na kiungo huyo wa kati ambaye aliwacha kipa wa wanabaharia hao, Wilson Oburu akidaka hewa.
Shaban Kenga alisawazisha katika dakika ya 27 baada ya kumeza krosi kutoka Ali Bai lakini dakika sita baadaye, Sofapaka walilejea uongozini pale mlinda ngome David Tavelu alipotia mpira ndani ya lango lake.
Ikiwa imebaki dakika 12 mchezo huu ukamilike, Sofapaka walipata la tatu wakati straika mkonge, John Baraza, alipofunga kutokana na krosi ya Anthony Kimani.
Lakini dakika nne kabla ya mechi kutamatika, Eric Okoth, alitia kimyeni la pili upande wa Bandari kuashiria pilka pilka kali za kutamatisha mechi hiyo.