MSANII maarufu wa vichekesho, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, anajipanga kutoa filamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Goodbye Mr. President’ akitarajiwa kumpa ‘shavu’ Rais Jakaya Kikwete (Pichani).
Akizungumza na Kabumbu Spoti jijini Dar es Salaam jana, Steve Nyerere alisema kuwa tayari ameshaandaa kila kitu, kilichobaki ni utekelezaji tu kwa wasanii kuingia katika maeneo watakayopangiwa kurekodi filamu hiyo, itakayokuwa na msisimko wa aina yake.
Steve alisema kwamba katika filamu hiyo, watacheza watu wengi wa kada mbalimbali na maarufu, wakiwamo wasanii wenye majina, viongozi wa ngazi mbalimbali za serikali, wabunge pamoja na waandishi wa habari wakongwe.
Aliongeza kuwa filamu hiyo itakamilika baadaye mwaka huu.
Baadhi ya filamu alizowahi kuzitoa ni pamoja na ‘Mwalimu Nyerere’, ‘My Son’, ‘Mke Mwema’, ‘Before Wedding’ na ‘Snake Kingdom’.