ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic, amejiunga na timu ya Al Jahra Sporting Club inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Kuwait.
Milovan alitimuliwa Simba kwa madai ya timu kutofanya vema katika mechi zake za Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya mtandao wa kijamii (Facebook), Milovan alisema anatarajia kwenda Kuwait kutoka nyumbani kwake Serbia alikokuwa amepumzika, kati ya leo au kesho.
“Nimefanikiwa kupata timu ya kuifundisha nchini Kuwait na kesho au kesho kutwa, naweza kuondoka, maana nimeishaanza kujiandaa kwa ajili ya safari,” alisema Milovan, kocha aliyeipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu msimu 2011/12.
