Mshambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 27 wa Sevilla, ambaye alikaribia kujiunga na
Atletico Madrid, lakini nia ya kuchezea timu inayofundishwa na Manuel
Pellegrini, City imeelezwa kumfanya abadili njia na sasa anakuja KLigi
Kuu ya England.
Fiti kabisa: Manuel Pellegrini anafikiri Alvaro Negredo atafaa Manchester City
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Hispania, alimaliza wa nne katika ufungaji bora wa
La Liga msimu uliopita kwa mabao yake 25 katika ligi hiyo, alitaka
kusajiliwa na Pellegrini wakati alipokuwa Malaga, lakini dili hilo
halikufanikiwa.
City
inataka kuboresha safu yake ya ushambuliaji baada ya kuwauza Mario
Balotelli kwenda AC Milan Januari mwaka huu na Carlos Tevez kwenda
Juventus mwezi uliopita.
Klabu
hiyo ilikuwa inamtaka mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani, ambaye
yuko mbioni kutua Paris St Germain kwa Pauni Milioni 50, dau ambalo
limemkatisha tamaa Pellegrini na sasa anaelekeza nguvu zake kwa Negredo,
aliyeanzia soka katika kikosi cha wachezaji wa akiba wa Real Madrid,
akiamini atafanya vizuri City.
Tajiri: City inatarajiwa kumkosa nyota wa Uruguay, Edinson Cavani
Ataondoka?: Atletico Madrid inaweza kumtaka mshambuliaji Edin Dzeko ikiwa watamkosa Negredo
Atletico
Madrid inaweza kuhamia kwa Edin Dzeko ikiwa watampoteza kwa
City, Negredo, mchezaji wa zamani wa mchezaji mpya aliyesajiliwa majira
haya joto, Jesus Navas.
Mshambuliaji
wa kimataifa wa Bosnia, Dzeko amekuwa pia akihuishwa na mpango wa
kuhamia Napoli kama mbadala wa Edinson Cavani anayeweza kutua PSG kwa
Pauni Milioni 53.However, Rafa Benitez is considering other targets.
Pellegrini
atafurahi Dzeko akibaki City, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
27 anataka kucheza na kuuzwa kwake, kutatoa nafasi kwa wengine kama
Negredo na beki wa Real Madrid, Pepe.