Mrembo huyo anamfanyia Essien kazi zake za
uhusiano ya jamii akiwa mkuu wa mfuko wa Essien ujulikanao ‘kama Michael
Essien Foundation’unaolenga kuimarisha huduma za kijamii nchini Ghana.
Lakini baada ya muda wa kazi, kumbe wawili hao ni
wapenzi wazuri na baada ya kuwa wapenzi wa muda mrefu kwa uhusiano wa
kimya kimya, Essien ameamua kuchukua mzigo jumla.
Akosua ameonekana katika Jiji la Accra
akirandaranda na pete ya ndoa ya Essien kitendo ambacho kinaashiria
kwamba wawili hao wamefunga ndoa.
Hivi karibuni, wawili hao walionekana wakila raha
katika hoteli ya Imperial Peking jijini Accra ambako Essien alikuwa na
kalamu maalumu ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuendesha mfuko wa
hisani kwa ajili ya kuchangia upatikanaji wa maji kijijini kwao.
Kabla ya hafla hiyo, jioni yake Essien aliandaa
mechi iliyowakutanisha mastaa kama Florent Malouda, Michael Ballack, Jay
Jay Okocha na wengine kwa ajili ya kuchangia mradi wake huo.
Imefahamika kuwa wakati uvumi ulipokuwa umeenea
mwaka mmoja uliopita kuwa Essien alikuwa amefunga ndoa na mwigizaji
maarufu wa Ghana, Nadia Buari katika sehemu moja ya siri jijini London,
kumbe aliyekuwa amefunga ndoa na Essien ni Akosua.
Imethibitika kwamba Essien na Akosua ni wanandoa
rasmi ambao wana watoto wawili wanaoishi nao Uingereza, jambo ambalo
limezua mjadala mkubwa ni kwa nini Essien aliamua kumtema Nadia ambaye
ni mrembo maarufu zaidi nchini Ghana?
Mjadala mkubwa uliopamba moto katika vyombo vya
habari vya Ghana ni ule ambao unajaribu kuwalinganisha Nadia na Akosua.
Maswali yanaulizwa kuhusu yupi kati yao ana mwonekano mzuri zaidi kwa
nje. Lakini pia maswali yamekuwa yakiulizwa kuhusu yupi kati yao ana
tabia njema za ndani ambazo zinaweza kumfanya awe mke wa mwanasoka
maarufu wa hadhi ya Essien ambaye anachukuliwa kuwa shujaa nchini kwao
Ghana.
Ni wazi kwamba chaguo la Essien kwa Akosua dhidi ya Nadia linamaanisha kwamba Essien ameangalia tabia zaidi ndani na si za nje.
Nadia ambaye ni mtoto wa mwanamuziki maarufu wa zamani wa Ghana, Sidiku Buari,anatajwa kuwa mrembo zaidi kuliko Akosua.