KOCHA Arsene Wenger amepewa ruhusa kuamua kuhusu usajili ya Pauni Milioni 40 wa Luis Suarez.Mshambuliaji huyo wa Liverpool ni kipaumbele cha kwanza katika usajili wa Arsenal majira haya ya joto na timu hiyo ya London tayari imetoa ofa ya awali ya Pauni Milioni 30 iliyokataliwa.
Gunners wameanza tena mazungumzo na mabosi wa Merseyside juu ya ofa mpya ya Pauni Milioni 35.
Lakini klabu hiyo ya Anfield imeweka wazi kwamba, mchezaji huyo hawezi kupatikana chini ya bei wanayoitaka.
Ofa ya Pauni Milioni 40 litakuwa jaribio tosha la kumng'oa Suarez anayetaka kuondoka Anfield majira haya ya joto.
Wakala wa Suarez, Pere Guardiola, alikuwa na majadiliano na Liverpool ambayo imekubali kusikiliza ofa.
Ofa hiyo itakuwa uamuzi mzito kwa Gunners ambao wanataka kumnasa mchezaji huyo mmoja kati ya watatu inayowataka sana.
Sambamba na Suarez, Wenger pia anafikiria kuwasajili Gonzalo Higuain na Wayne Rooney