Wajumbe
wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
utakaofanyika Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) wanawasili jijini Dar es
Salaam kesho (Julai 12 mwaka huu).
Mkutano
huo wa marekebisho ya Katiba utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais wa TFF,
Leodegar Tenga na utafanyika ukumbi wa NSSF Waterfront kuanzia saa 3
kamili asubuhi. Wajumbe wote wa mkutano huo watafikia hoteli ya
Travertine.
Pia
mkutano huo utahudhuriwa na wageni mbalimbali waalikwa wakiwemo kutoka
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na Chama cha Mpira wa
Miguu Zanzibar (ZFA).
UGANDA CRANES YAWASILI KUIKABILI STARS
Timu
ya Taifa ya Uganda (The Cranes) imewasili Dar es Salaam leo tayari kwa
mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa
Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) kati yake na Tanzania (Taifa Stars)
itakayochezwa Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
The
Cranes inayofundishwa na Mserbia Sredojvic Micho imetua Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air
Uganda, na imefikia hoteli ya Sapphire.
Timu
hiyo leo (Julai 11 mwaka huu) itafanya mazoezi saa 9 alasiri kwenye
Uwanja wa Karume, wakati kesho saa 9 alasiri itafanya mazoezi Uwanja wa
Taifa, kabla ya kuipisha Taifa Stars itakayoanza mazoezi saa 10 kamili
jioni.
Taifa
Stars inayofundishwa na Mdenmark Kim Poulsen, na kudhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager, leo kwa mujibu wa program yake haitakuwa na
mazoezi.
Wachezaji
wanaounda The Cranes ni makipa Ismail Watenga, Kimera Ali na Muwonge
Hamza. Mabeki ni Guma Dennis, Kasaaga Richard, Kawooya Fahad, Kisalita
Ayub, Magombe Hakim, Malinga Richard, Mukisa Yusuf, Savio Kabugo na
Wadada Nicholas.