Kujenga viwanja vyenye air-condition na vyenye uwazi kwa juu katika jangwa ni gharama sana.
Kampuni ya Deloitte imesema kwamba Qatar itatumia $200 billion katika kipindi cha miaka 10 ijayo wakati ikijiandaa kuandaa 2022 World Cup, the Associated Press imeripoti.
Fedha
hizo zitatumika kwenye miundombinu ya usafiri na utalii pamoja na
viwanja vipya. Zaidi ya mashabiki 400,000 wanategemewa kwenda kwenye
nchi hiyo kwa ajili ya michuano hiyo itakayochukua mwezi mmoja
kufanyika.
Wakati
michuano hiyo ikipangwa kufanyika kwenye wakati wa kiangazi, joto
hupanda kwa kiasi kikubwa sana, Qatar inajipanga kujenga viwanja vyenye
air-condition, pamoja na vyenye uwazi kwa juu ambavyo vyote vitakuwa
vikitumia umeme wa nguvu za jua.