MBRAZIL Neymar na Muargentina, Lionel
Messi wataunda pamoja safu kali ya ushambuliaji ya Barcelona msimu ujao,
lakini walikuwa timu tofauti leo katika mechi ya Hisani nchini Peru.
Nyota hao wa Amerika Kusini, waliungana
na wakali kama Daniel Alves, Ezequiel Lavezzi, Javier Mascherano na Eric
Abidal kwa mechi hiyo baina ya Messi na marafiki zake dhidi ya
wachezaji wengine duniani.
Karibu sana: Lionel Messi (kulia) na Neymar


Vijana wa Barca: Lakini Neymar na Messi walikuwa timu tofauti katika mechi hiyo ya hisani
Ilikuwa mara ya kwanza wanakutana
uwanjani tangu gwiji wa Barca, Johan Cruyff ashauri mshindi mara nne wa
Balon D'or, Messi auzwe kumuachia nafasi mchezaji mwenzake mpya
aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 50.
Na Neymar alimgaragaza Messi, ambao wote walivaa jezi namba 10 katika mechi hiyo, kwa kufunga bao la umbali wa mita 45.
Na baadaye akamnyanyasa beki wa Malaga na Uruguay, Diego Lugano.
Lakini Messi ndiye aliyeibuka kifua mbele mwishowe kwa timu yake kushinda 8-5.
Fedha zote zitakazopatikana katika
mchezo huo, zitakwenda kwenye mfuko wa kujenga mustakabali mzuri wa
maisha kwa watoto kimataifa.

Mwenye mpira: Neymar, kushoto, akimtoka Muargentina, Javier Mascherano, kulia,

Mtu wa mbele: Lionel Messi, kushoto, ameandaa mechi ya Hisani Peru

Marafiki wameungana: Messi na Daniel Alves, Ezequiel Lavezzi na Eric Abidal