STAA kwenye kiwanda cha muziki wa kizazi kipya Afrika mashariki Prezoo (Pichani) kutoka Kenya jana amemnaga hadharani staa mwenzake toka Tanzania Naseeb Abdul 'Diamond' kwa kitendo chake cha kumtaka amuombe radhi kupitia kurasa yake ya Twitter.
Prezoo amedai hakuna haja ya majibizano na amemtaka Diamond kupuuuza yote aliyoyasikia kwani wanaume huwa hawagombani, Kuhusu yeye kuomba radhi hilo halipo kwani anaona kama utoto, Msanii huyo ameendelea kusema masuala ya kuombana radhi kwenye twitter yamepitwa na wakati na anachoangalia yeye ni maisha yake ya kimuziki.
Aidha amedai kuwa ana bifu na Diamond na amewataka mashabiki wake kuendeleza amani na msanii huyo, Diamond alitangaza hadharani aombwe radhi na Prezoo kutokana na kutokea tofauti kati yao kitendo ambacho kimepingwa vikali na Prezoo
