come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Ripoti za fedha kuziengua klabu Ligi Kuu

Shirikishola Soka (TFF) limezitaka klabu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara kuwasiliana ripoti ya mwaka jana ya mapato na matumizi ya fedha kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa ligi.
Akisoma hotuba katika hafla ya kukabidhi zawadi za ubingwa wa msimu uliopita iliyofanyika jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia jana, katibu mkuu wa shirikisho hilo, Angetile Osiah alisema klabu ambazo hazitawasilisha ripoti zake, hazitaruhusiwa kushiriki ligi hiyo.

"Lengo letu ni kuhakikisha tunakwenda kisasa zaidi sambamba na kutekeleza maagizo ya FIFA (Shirikisho la Soka la Kimataifa) ambao wanataka klabu ziwe 'audited' (zikaguliwe). Watakaoshindwa kuleta ripoti ndani ya muda huu, hawataruhusiwa kushiriki ligi itakapoanza," alisema Osiah.

Aidha, katibu mkuu huyo ambaye alikuwa amemwakilisha Rais wa TFF, Leodegar Tenga, alizitaka klabu 14 zinazoshiriki ligi hiyo kupeleka majina ya viwanja vyake vya mazoezi kabla ya kuanza kwa msimu ujao ili kutimiza masharti ya usajili wa klabu, kipengele ambacho kiliingizwa kwenye katiba ya TFF mwishoni mwa mwaka jana kufuatia maagizo ya Chama cha Soka Afrika (CAF).

Msimu wa 2013/14 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utaanza Agosti 24 ukishirikisha timu za Yanga, Azam, Simba, Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Coastal Union, Ruvu Shooting, JKT Oljoro, JKT Ruvu, Tanzania Prisons, Mgambo JKT, Mbeya City, Rhino Rangers na Ashanti.

Maagizo hayo yanaonyesha dhamira ya TFF ya kuhakikisha klabu zinafanyiwa ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha kwani utaratibu huo umekuwa ukikiukwa kwa muda mrefu. TFF yenyewe ilikaguliwa kwa mara ya mwisho na Mamlaka ya Mapato (TRA) 2010 kabla ya kukaguliwa tena mwanzoni mwa mwaka huu.

Hata hivyo, malipo ya mapato ya milango kwa klabu na serikali yanafanywa kwa pesa taslim.