|
|
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 24, awali akichezea Corinthians, alicheza sana katika kikosi cha kwanza cha Brazil wakati wa mechi za Kombe la Confederations ambalo hatimaye taifa hilo lilimaliza kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Uhispania katika fainali Jumapili.
Tottenham haikufichua maelezo kuhusu bei aliyonunuliwa na wala muda wa mkataba aliotia saini.
Aliambia akaunti rasmi ya Twitter la klabu hiyo ya London kaskazini, @SpursOfficial: "Nina furaha sana na msisimko kujiunga na Spurs. Ni furaha kubwa katika uchezaji wangu kuwa katika klabu kubwa hivi kama Tottenham."
Inter Milan na Real Madrid walikuwa wameaminika kuwa walikuwa wakitaka kumsaka kiungo huyo wa kati, ambaye alifunga mabao mawili wakati wa Kombe la Confederations, baada yake kufungia Brazil mechi ya kusawazisha wakati wa sare ya 2-2 dhidi ya Uingereza mwezi uliopita.