come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Uhispania warejea darasani



Juni 16, 2010 na Juni 30, 2013.
Ni tarehe ambazo kati yake zinaweka kwa mabano kipindi cha ubabe ambacho kilifikia kikomo Jumapili mjini Rio kwa mabingwa wa dunia Uhispania kwani rekodi yao ya kutoshindwa mechi 29 ilihitimishwa kwa kichapo cha 3-0 kwenye fainali ya Kombe la Confederations mikononi mwa Brazil.

Kwenye kipindi hicho cha miaka mitatu na wiki mbili, Furia Roja walikuwa wamefanikiwa kuwa timu ya kwanza katika soka ya kimataifa kushinda dimba tatu kuu mtawalia, baada ya kuongeza Kombe la Dunia 2010 na Euro 2012 kwenye ushindi wao wa Euro 2008.
Vyombo vya habari vya Uhispania vilisifu enzi hiyo kama iliyodhihirisha kwamba Wahispania si watu wa kushindwa kila wakati.
Lakini huku wakitakiwa kutetea taji lao la dunia mwaka mmoja ujao, Vicente del Bosque na wenzake watalazimika kurudi darasani.
Del Bosque alikiri kuwa Brazil walikuwa bora kuwashinda siku hiyo – Uhispania walionekana wachovu na waliolemewa kabisa baada ya Fred kufungia wenyeji bao la ufunguzi dakika ya pili kabla ya Neymar na Fred kumaliza mambo mechi hiyo iliyoegemea upande mmoja.
"Walistahiki, wakati mwingine ni muhimu kushindwa,” alisema Del Bosque.
"Bila shaka hatuna raha lakini lazima tutathmini kujua nini kilienda kombo. Hata hivyo, rekodi yetu inatutia moyo … tuna wachezaji wazuri na mtindo maalum wa kucheza.
“Huwa huwezi kubadilisha hayo yote eti kwa sababu umeshindwa mara moja, hata ilivyostahiki,” alisema kocha huyo wa zamani wa Real Madrid kwa utulivu baada yake kushinda kuibuka kocha wa kwanza kushinda Kombe la Dunia, Ubingwa Ulaya, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Kombe la Confederations – tayari yuko peke katika kushinda mataji ya kwanza matatu.
"Soka ni mchezo na tulijua wapinzani wetu walikuwa na nguvu sana na mambo yalifaa kuanzia mwanzo” kufuatia bao la Fred mwanzoni mwa mechi, alisema Del Bosque.
Difenda wa Real Madrid Sergio Ramos alikubali kuwa “ilikuwa na zile siku ambazo kila kitu hukukataa. Ilikuwa jambo mbaya kufungwa mapema ukizingatia tulikuwa tumefika fainali tukiwa na matumaini makubwa,” alisema Ramos, ambaye penalti yake aliyopoteza ilikuwa moja ya mikosi ambayo ilidhihirisha kwamba haikuwa siku njema kwao.
"Inatubidi tu tuwasifu wapinzani wetu kwa mchezo wao mzuri, na leo tuliona upande mwingine wa sarafu ya soka – lakini huwezi kufanikiwa kila wakati.”
Kiungo wa kutegemewa sana upande wa Uhispania, Andres Iniesta, pia alikuwa na siku mbaya huku Brazil wakiwalemea wapinzani wao.
Lakini mchezaji mwenzake wa siku zijazo Barcelona Neymar alisema: "Hiyo ni soka, lazima ujikwamue. Walikuwa bora na walituzungusha. Mwaka ujao tutarudi tena na tunatumaini kufanya vyema zaidi.”
Licha ya wachezaji wenzake kuwa na matumaini, nahodha Iker Casillas alisema avunjwa moyo, na hali kwamba Uhispania ilishindwa kushinda taji ambalo halimo kwenye rafu yake.
“Kushinda huko kunauma. Tunaweza tu kusema heko Brazil na kufunganya virago vyetu.”
Difenda wa Barcelona Gerard Pique, aliyetumwa nje ya uwanja kipindi cha pili baada ya kumchezea visivyo Neymar, alisema baadaye kwamba kulikuwa na jambo la kujivunia kutoka kwa mechi hiyo ya jioni.
"Neymar ni mchezaji hodari. Nina furaha kwamba atakuwa akichezea timu yangu msimu ujao,” Pique alisema.