come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Baraza alenga matokeo mem

Francis Baraza 

Kocha wa Western Stima, Francis Baraza, anaamini kwamba kikosi chake kitajiondoa kutoka lindi la utepetevu ambao uliwafanya wamalize awamu ya kwanza ya Ligi Kuu Kenya katika nafasi ya 11.

Baraza anatazamia kikosi chake kitatia fora katika muhula wa pili wa shindano hilo baada ya kuzoa alama 17 katika mkondo wa kwanza kufuatia ushindi wa mechi nne, sare tano na kushindwa mara sita.
Mwalimu huyo anadokeza bado azima yao ya kutwaa taji iko hai kwani viongozi Thika wamefanikiwa kupata alama 26 kufikia sasa na amepatia kikosi chake changamoto ya kufunga huo mwanya.
“Shindano hili ni kali sana lakini tunakiri tumekuwa hafifu kwa muda sasa. Baadhi ya makosa tulioyafanya katika mwanzo wa musimu yalitugharimu alama muhimu.
“Tunatarajia kuandikisha ushindi na kupanda ngazi ya ligi. Tunaelewa hili halitakuwa rahisi kwani kila timu inawania taji hili lakini nina uhakika tukitia bidii, tutafanikiwa,” Baraza alisema.
Stima watawaalika KCB katika mechi yao ya kwanza ya mkondo wa pili Jumapili.