Timu ya Ligi Kuu Kenya Ulinzi Stars wako tayari kukabiliana
vilivyo na Ufaransa katika mechi yao ya ufunguzi katika kinyanganyiro
cha Kombe la Dunia la Majeshi Jumanne huko Baku, Azerbaijan.
Mkufunzi wao, Salim Ali alieleza wanadhamiria kushinda wapinzani wao ili kuwapa motisha wa kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.
“Kila kikosi kinalenga kutwaa taji hili na ni muhimu tuandikishe matokeo ya nguvu katika mechi yetu ya kwanza na kulingana na matayarisho yetu, tunatarajia kuanza kwa kasi,” Ali alisema.
Kenya na Ufaransa wamo katika kundi B pamoja na Bahrain na Algeria. Wachezaji 18 walisafiri kwa kikosi chao miongoni mwao wakiwa Francis Ochieng, James Saruni na Francis Onyiso katika lango.
Ngome yao itadhibitiwa na Kelvin Ouma, Josiah Okello, Oliver Kipruto, Mohammed Hassan, James Mulinge na Geoffrey Kokoyo, ilhali, Lawrence Owino, Stephen Ochollah, Erick Apul, Kelvin Simiyu, Chester Okoyo, Salim Mohammed na Kelvin Amwayi ndio viungo wa kati.
Mashambulizi yataongozwa na Evans Amwoka na Stephen Waruru.