UONGOZI wa Yanga SC, chini ya Mwenyekiti, Aljah Yussuf Manji leo unatimiza mwaka mmoja madarakani. Kufuatia kujiuzulu kwa viongozi wakuu, Mwenyekiti, Wakili Lloyd Nchunga, Makamu wake Davis Mosha, Yanga ililazimika kuitisha uchaguzi wa kujaza nafasi hizo na Julai 14 Manji akachaguliwa kuwa Mwenyekiti na Clement Sanga Makamu wake.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, kulikuwa kuna nafasi nne pia za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji za kujazwa na Abdallah Bin Kleb, Mussa Katabaro, George Manyama na Aaron Nyanda
Yanga bado hawana hata Uwanja wa mazoezi na hosteli ya klabu, makao makuu Jangwani ipo katika hali mbaya. Mwaka umekatika na hakuna dalili za klabu kuanza kujiendesha kibiashara zaidi ya kubaki kuwa tegemeo.
Uongozi mpya Yanga, umeshindwa japo kuvutia makamapuni mapya kuidhamini klabu zaidi ya TBL, ambayo iliingia wakati Mwenyekiti wa klabu akiwa Imani Madega mwaka 2008.
Wakati Mohamed Dewji anaifadhili Simba SC alizivutia pia na benki za NBC na kampuni ya Tanga Cement kuidhamini klabu hiyo.