come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Zico azingatia kibarua Sony

Zedekiah Otieno

Mwalimu Zedekiah ‘Zico’ Otieno bado ana azima hajakamilisha katika kilabu cha Ligi Kuu Kenya na anatazamia kufanya vyema baada ya kurejea tena kama kinara wa timu hiyo.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Harambee Stars alirejea katika vijana hao wenye asili ya Awendo miezi sita tangu kujiuzulu kwa sababu za kibinafsi.
Atachukua mahala pake Sammy Omollo ambaye amewacha timu hiyo ikidorora katika Ligi Kuu, alama tatu pekee mbele ya eneo la kuchushwa daraja.
Otieno amekiri kwamba kukiinua kilabu hicho itakuwa kibarua kigumu lakini hana budi ikitiliwa maanani hadhi ya timu hiyo.
“Sony Sugar ni kilabu kikubwa na hakifai kumiliki nafasi waliomo sasa. Kuinua hadhi yao haitakuwa rahisi lakini ni jukumu linalotakikana. Ligi imekabana na kupanda ngazi ni kizungumkuti lakini azima yetu ni kufanya juhudi zote kumalizia katika nafasi njema.
“Mechi zilizosalia ni mingi kubadilisha taswira na nitafanya kila niwezalo kutekeleza hilo,” Otieno alisema.
Kocha huyo alikuwa mkufunzi wa kilabu cha Daraja la Kwanza, Mahakama katika awamu ya kwanza ya musimu huu.