come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

Lavatsa aridhishwa na imani ya mkufunzi Kenya

Edwin Lavatsa

Mshambulizi Edwin Lavatsa amerithishwa na imani mkufunzi mkuu wa Harambee Stars Adel Amrouche aliyonayo na uwezo wake.

Licha ya shinikizo la kumpatia nafasi mchezaji mwingine, Lavatsa amebaki kama kigezo katika kikosi cha Amrouche tangu achukue mamlaka ya timu ya Taifa ilhali mshambulizi huyo hajakuwa akiongoza orodha ya mabao katika Ligi Kuu Kenya.
Imani hiyo ililipwa maridhawa Jumanne pale Lavatsa alipoibuka kama nyota wa Stars na mabao yote mawili katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Swaziland katika dimba la mataifa bingwa Afrika Kusini kuipa Kenya kipao mbele katika kundi lao la B.
Kejeli ni kwamba Amrouche aliathimisha ushindi wa kwanza kama mwalimu wa Stars katika mechi hiyo.
“Kufungia kikosi cha Taifa ni radhi kwa kila mchezaji kwani juhudi zetu za kila siku ni kutimiza azimio hilo.
“Nashukuru wenzangu kwa kunisaidia kungara kwani bila wao, singeliweza kufanya vyema kadili ya nilivyofanya. Kocha amedhihirisha imani yake kwangu na ninarithishwa kurahisisha jukumu lake,” Lavatsa alisema.
“Bado tuna kibarua cha tutimiza na ni lazima tuzidishe bidii katika mechi yetu ya mchujo ya mwisho ili tufuzu kwa robo fainali. Lengo letu ni kuendelea kwa dimba hili kadili ya uwezo wetu kwa hivyo, hatuwezi sherehekea sasa,” aliongeza.
Stars watakabiliana na Botswana Alhamisi ambapo ushindi utahakikisha kufuzu kwao kwa mechi dhidi ya Angola katika robo fainali.