come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

DISKO TOTO YAPIGWA MARUFUKU SIKUKUU YA IDDI

HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam, imetoa onyo kwa wamiliki wa kumbi za starehe kutopiga disko kwa watoto ‘Disko Toto’ au kubandika matangazo kuhusu shughuli hizo kuelekea Sikukuu ya Idd.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Ofisa Utamaduni wa halmashauri hiyo, Shani Kitogo, alisema kwa yeyote atakayekiuka atafuatiliwa na kuchukuliwa hatua, si kipindi cha sikukuu tu bali hata baada ya kumalizika.

“Sheria ya Wizara ya Viwanda na Biashara ya vilevi, hairuhusu mtoto mdogo kuingia katika kumbi zinazouza vilevi, lakini cha kushangaza, baadhi ya wamiliki wamekuwa wakikiuka sheria hiyo huku wakijua wazi kuwa ni makosa,” alisema.