
Katika mchezo huo wa kwanza hatua ya 32 Bora, Mtaliano huyo alifunga bao lake hilo la kwanza dakika ya 15 tangu ajiunge na klabu hiyo Januari baada ya kumtoka beki Jose Fonte.
Katika mchezo mwingine, Jonathan Soriano alifunga katika ushindi wa Salzburg dhidi ya Ajax mabao 3-0 mjini Amsterdam.
Soriano alifunga mara mbili la kwanza dakika ya 14 kwa penalti na la pili dakika ya 35 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Ajax, Jasper Cillessen na lingine likafungwa na Sadio Mane.
Roman Bezjak alifunga bao la ushindi katika mchezo ambao timu zote zilikosa penalti na zote kupoteza wachezaji kwa kadi nyekundu.
Wageni walikosa penalti dakika ya nane kupitia kwa Svetoslav Dyakov, na Felipe Anderson akapoteza nafasi ya kuisawazishia Lazio dakika tano tangu kuanza kipindi cha pili.
Dyakov alitolewa kwa kadi nyekundu dakika tano baadaye, lakini idadi ikaongezeka baada ya Luis Cavanda kutolewa pia nje dakika ya 73.
Eintracht Frankfurt ilitoka nyuma kwa mabao mawili na kupata sare ya 2-2 na Porto.
Mabao ya kila kipindi ya Ricardo Quaresma na Silvestre Varela yaliiweka mbele timu ya Ureno, lakini Joselu akapunguza moja dakika ya 72 kabla ya Alex Sandro kujifunga dakika sita baadaye na kuwapa Wajerumani hao sare ya ugenini.

Eduardo Vargas na Sofiane Feghouli, wote wakiingia kipindi cha pili walifunga katika dakika za 80 na 90 na kuiweka barabarani timu hiyo ya Hispania katika mbio za taji hilo la Ulaya.
Mechi hiyo ilichezwa mjini Nicosia, Cyprus, kwa sababu ya vurugu zinazoendelea katika Jiji hilo la Ukraine .
Fiorentina pia iliifumua mabao 3-1 Esbjerg, Alessandro Matri akiifungia timu hiyo ya Serie A bao la kwanza dakika ya nane, kabla ya Martin Pusic kusawazisha dakika mbili baadaye, Josip akafunga la pili dakika ya 15 kwa Wataliano hao.
Alberto Aquilani akafunga la tatu kwa penalti kabla ya mapumziko na kuivusha mguu mmoja mbele hatua ya 16 Bora La Viola.
Sevilla ilitoa sare ya 2-2 na Maribor ikitoka nyuma kwa mabao 2-1.
Marcos Tavares aliwafungia Waslovenia bao la kuongoza, lakini jitihada za kipindi cha pili za Kevin Gameiro na Federico Fazio zikabadilisha matokeo.
Bao la dakika ya 81 la Yevhen Konoplyanka kwa penalti liliipa Dnipro ushindi wa 1-0 dhidi ya Tottenham nchini Ukraine.
Timu nyingine ya Ukraine, Shakhtar Donetsk pia itakuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano baada ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Viktoria Plzen.
Stanislav Tecl aliifungia bao la kuongoza timu ya Czechs dakika ya 62, lakini Luiz Adriano akasawazisha dakika nne baadaye.
Rubin Kazan waliomaliza 10 walipata sare ya 1-1 ugenini na Real Betis, licha ya Alexander Prudnikov kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 28.
Wakati huo tayari Betis wanaongoza kwa bao la Didac Vila, lakini Roman Eremenko akasawazisha kwa penalti dakika ya 74.

Mechi baina ya Chornomorets na Lyon na Anzhi Makhachkala na Genk ziliisha kwa sare ya bila kufungana, huku Anzhi ya Urusi ikimaliza mchezo na wachezaji 10 kufuatia Ilya Maksimov kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 89.
Mechi baina ya Swansea na Napoli na Maccabi Tel-Aviv na Basle pia ziliisha kwa sare ya 0-0.