Na Regina Mkonde
Wachezaji wa kutumainiwa wa ambingwa wa soka nchini Yanga wamesema kuwa kikosi cha Ruvu Shooting cha Mlandizi mkoani Pwani kesho kiwasamehe kwa dhahama ya magoli watakayopawa katika mchezo wa ligi kuu ya bara mzunguko wa pili raudni ya 19.
Yanga itacheza na Ruvu Shooting katika uwanja wa Taifa huku vijana wa Ruvu wanaonolewa na Mkenya Tom Olaba wakijitamba kushinda, lakini Mrisho Ngasa mfungaji wa Yanga dhidi ya Komorozine magoli 5 amedai Ruvu Shooting iwasamehe kesho kwani ameapa kutoka na goli zaidi ya tatu peke yake.
Wakati Ngasa akijitamba hivyo, Didier Kavumbagu naye ametamba kutoka na goli mbili katika mchezo huo ili kupigania mbioza ufungaji bora, lakini kiungo mchezeshaji Athuman Idd 'Chuji' yeye amesema lazima Yanga itoke na ushindi mkubwa ili kuitisha Al Ahly ya Misri ambayo watakutana nayo Machi mosi mwaka huu.
Kauli hizo zinawapa faraja mashabiki wa Yanga ambao wameanza kuingiwa na hofu hasa kufuatia msemaji wa Ruvu SDhooting Masau Bwire kutamba kuibuka na suhidni dhidi ya Yanga kesho, wachezaji hao wa Yanga waliendelea kujifua huko Bagamoyo na watawasili jijini kwa ajili ya mechi hiyo leo