![]() |
|
|
|
Fulham watakuwa wakijaribu kuweka vituko vya nje
ya uwanja nyuma na badala yake kuangazia vita vyao vya kujaribu kukwepa
shoka la kushushwa ngazi watakapotembelea wenzao wanaohangaika West
Bromwich Albion katika Ligi ya Premia Jumamosi.
Klabu hiyo ya London magharibi ndiyo inayoshika mkia ikiwa na alama 20, nne kutoka eneo salama, na Ijumaa waliteua Mjerumani Felix Magath kuwa meneja wao wa tatu msimu huu baada ya kufuta Martin Jol na Rene Meulensteen.
Klabu hiyo ilithibitisha wiki hii kwamba kocha msaidizi Ray Wilkins na mkurugenzi wa kiufundi Alan Curbishley walikuwa wamefutwa, wiki chache tu baada yao kuteuliwa, huku makocha wa timu ya kwanza coaches Mick Priest na Jonathan Hill pia wakijiunda na wakufunzi ambao wameondoka Craven Cottage.
.
Fulham, ambao wamekuwa kwenye Ligi ya Premia tangu 2001, wamepata alama moja pekee kutoka kwa mechi zao sita walizocheza majuzi na wamemchukua Magath wakitumai kwamba atamaliza masaibu yao.
“Tutapata ujuzi na uzoefu wake Ujerumani na bila shaka ninafikiri atatusaidia kutimiza lengo letu la kukaa katika Ligi ya Premia,” kiungo wa kati na Mjerumani mwenzake Lewis Holtby alisema.
Mchezaji Kostas Mitroglou aliyenunuliwa kwa kuvunja rekodi huenda akawachezea mechi yake ya kwanza baada ya kutua huko kutoka kwa mabingwa wa Ugiriki Olympiakos Piraeus akiwa hayuko sawa kucheza.
West Brom wamo nje ya eneo la kushushwa ngazi kwa wingi wa mabao, na licha ya sare muhimu ya 1-1 dhidi ya Chelsea mechi yao iliyopita, hawajashinda chini ya meneja mpya Pepe Mel.
Manchester City watakuwa wakilamba vidonda vyao walivyopata walipolazwa na Barcelona Jumanne katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya watakapokuwa wenyeji wa Stoke City Jumamosi (1500), mechi yao ya mwisho kabla ya kukutana na Sunderland katika fainali ya League Cup Machi 2.