come

come
Tuletee habari za kijamii, michezo na burudani, email kabumbu1935@gmail.com

REAL MADRID YATAREMSHWA KILELENI LA LIGA

MWANASOKA bora wa dunia, Christiano Ronaldo alimkasirikia Gareth Bale jana wakati Real Madrid ikifungwa kwa mara ya pili ndani ya siku nne katika La Liga na kupigwa kumbo na Barcelona na Atletico Madrid katika mbio za ubingwa.

Huku Real ikichapwa mabao 2-1 na Sevilla, Ronaldo alishindwa kuficha hasira zake baada ya mwanasoka ghali duniani, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 86, Bale alipoamua kupiga mpira wa adhabu, badala ya kumuachia mshambuliaji huyo Mreno, na akaenda kupiga juu ya lango.

Ilikuwa ni siku mbaya kwa mwanasoka huyo wa Wales, ambaye alitoka uwanjani mara moja kwenda kubadilisha viatu na kuiacha Real ikiwa pungufu na wachezaji 10. Wakati anabadilisha viatu, Carlos Bacca ndipo alipoifungia bao la ushindi Sevilla dakika ya 73.


Kipigo cha Madrid Uwanja wa Sanchez Pizjuan jana, kinakuja siku nne baada ya kufungwa na Barcelona, Lionel Messi akimfunika Ronaldo kwa kufunga hat trick katika ushindi wa 4-3 mjini Madrid.

MATOKEO YA MECHI ZA JANA LA LIGA
Atletico Madrid 1 Granada 0
Barcelona 3 Celta Vigo 0
Sevilla 2 Real Madrid 1
Vipigo hivyo mfululizo,vinakuja baada ya timu ya Carlo Ancelotti kucheza mechi 31 mfululizo bila kupoteza hata moja.

"Tunatakiwa kuendelea kufanya kazi, kupambana na kuwaomba msamaha mashabiki wetu,"alisema beki wa pembeni wa Madrid, Marcelo.

Bacca alikuwa kondakta wa basi za nchini mwao mwanzoni mwa umri wake wa miaka ya 20,kabla ya mambo kumnyookea kwenye soka.

Mshambuliaji huyo wa Columbia alitua Sevilla kwa Pauni Milioni 6 msimu huu na sasa amekwishafunga mabao 18 kwenye mashindano yote msimu huu.

Alikuwa shujaa wa mchezo baada ya kipindi cha kwanza pia kufunga bao la kwanza dakika ya 19 kwa pasi ya Jose Antonio Reyes na kipindi cha pili alifunga kwa pasi ya Ivan Rakitich, kiungo wa Croatia aliyemtoka vizuri Pepe na kumpasia Bacca aliyemtungua kipa Diego Lopez kukamilisha ushindi wa 2-1. Ronaldo alifunga bao la Real dakika ya 14.

Huku Atletico Madrid ikiifunga Granada 1-0, bao pekee la Diego Costa dakika ya 63, nayo Barcelona iliitandika 3-0 Celta mabao ya Neymar dakika ya sita na 67 na Messi dakika 30.

Matokeo hayo, yanaifanya Atletico inayofundishwa na kocha Diego Simeone ipae kileleni mwa Liga kwa kufikisha pointi 73, Barcelona iliyofikisha pointi 72 sasa ya pili na Real inayobaki na pointi zake 70 inakuwa ya tatu.