|
|
Manuel Pellegrini amepuuza Chelsea kama ‘timu
ndogo’ na kubashiri mengi zaidi kutoka nyota mkongwe Frank Lampard baada
ya timu yake Manchester City kutoka sare ya 1-1 na Chelsea.
Mabingwa hao wa Uingereza walinusuru alama kupitia Lampard ambaye anashikilia rekodi ya mabao Chelsea ikisalia dakika nne muda wa kawaida kuisha baada ya kupunguzwa kuwa wachezaji kumi baada ya beki Pablo Zabaleta kupewa kadi nyekundu.
Kiungo wa akiba, Andre Schurrle, alipatia Chelsea uongozi dakika chache baada ya Zabaleta kuondoka kabla ya Lampard kutoka benchi na kupokewa kwa makofi kutoka mashambiki wote ugani Etihad.
Na kama mswada wa filamu, Lampard, 36, alikomboa goli hilo huku akichezea City kwa mkopo baada ya kusaini na klabu cha Marekani, New York City, ambacho kinamilikiwa na mabingwa hao wa Premier baada ya kutumikia Chelsea kwa miaka 13.
“Sikuwa na tashwishi angekuwa muhimu kwetu kwani ni mchezaji mkongwe na mwenye ubora. Ilikuwa muhimu kwake kuendelea kufanya kazi kila siku kwani hakuwa na lolote kufanya New York hadi Januari musimu unapoanza huko,” Pellegrini alisema.
Meneja huyo alishambulia mbinu za Chelsea akizilinganisha na zile za Stoke City na kuziita mipango ya ‘timu ndogo’.
“Tulicheza na timu kama Stoke kulingana nami,” alisema.
Mwenzake Mourinho ambao amekuwa na uhusiano wa baridi na Pellegrini baada ya kumridhi kama kocha wa miamba wa Uhispania, Real Madrid, 2010 alikataa kuingia kwenye mtego wa kurushiana maneno.
“Tumeshinda alama moja hapa kwani tulitembelea mabingwa na mbili mbele ya wanaotufuata karibu lakini tumeweza kutoka na uongozi wa alama tatu.
“Mara mingi, Pellegrino husema hazungumzi juu yangu au timu yangu lakini anaendelea kurusha maneno. Sitamjibu, msiniulize juu yake, sina haja na hayo,” Mourinho, ambaye alitamka vibaya jina la mwalimu mwenzake kimakusudi, alisema.